Friday, April 17, 2015

KIJUE CHA UALIMU CHA ERA KINACHOMILIKIWA NA PASKAZIA BARONGO

 Mkurugenzi wa chuo cha ualimu cha ERA, Paskazia Barongo, kiko eneo la Kagemu lililoko katika kata ya Kitendagulo, katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha REA wakiwa darasani.
 Mkrugenzi akiwa amesiamam nje ya moja ya vyumba vya madarasa ya chuo hicho.
 Mmoja wa walimu katika chuo cha ERA.
 Mandhali ya chuo cha ERA.


Thursday, April 16, 2015

Mwandishi Ukraine auawa kwa risasi


Oles Buzyna mwandishi wa habari maarufu aliyeuawa nchini Ukraine
Mwandishi maarufu wa Ukraine ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Kiev na watu waliokuwa wameficha nyuso zao.
Oles Buzyna alifahamika sana kwa maoni yake ya kuunga mkono Urusi na amefanya kazi ya uchapishaji akishirikiana na serikali ya rais Viktor Yanukovych aliyeondolewa madarakani nchini Ukraine.
Kifo chake kimekuja siku moja baada ya mwanasiasa mwenye kupendelea Urusi, Oleh Kalashnikov kuuawa katika shambulio linalofanana.
Rais Poroshenko ametaka uchunguzi ufanyike haraka, amesema mauaji haya dhidi ya watu maarufu yamefanyika makusudi na maadui wa Ukraine.

David Cameron akwepa mdahalo wa pili


Viongozi wa vyama vitano vya upinzani wameshiriki katika mdahalo wa pili wa moja kwa moja ulioandaliwa na BBC.
Katika hoja za kwanza, kiongozi wa chama cha Labour, Ed Miliband, amesema suala la familia za wafanyakazi atalipa kipaumbele kwanza, wakati kiongozi wa UK Independence Party,UKIP, Nigel Farage amesema atasaidia biashara ndogo ndogo. Nicola Sturgeon kiongozi wa chama cha Scotish National Party amesema anataka kuona muungano wa Uingereza unakuwa bora zaidi katika kila sehemu ya nchi hiyo. Viongozi wa Plaid Cymru na Green Party pia nao wameshiriki katika mdahalo huo.
Bwana Miliband, amesema anatarajia kupata ushindi mkubwa na hataunda serikali ya mseto na chama cha SNP.
Wagombea hao wamekuwa wakipingana katika masuala mbalimbali wakati wa mdahalo huo.
Waziri mkuu David Cameron wa chama tawala cha Conservatives na naibu waziri mkuu wake kutoka chama cha Lib Dem, Nick Clegg hawakushiriki katika mdahalo huo wa wazi.

Gesi ya chlorine yatumika Syria


Mtoto aliyeathirika na shambulizi la kemikali
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limetoa kanda yenye ushahidi inayoonyesha matumizi ya gesi ya chlorine kwenye shambulizi moja mwezi uliopita nchini Syria.
Kanda hiyo inaonyesha watoto watatu walio chini ya miaka minne ambao walikufa licha ya kuwepo jitihada za kuwakoa.
Daktari raia wa Syria ambaye aliwatibu watoto hao kwenye hospitali moja iliyo mkoa wa Idlib aliuambia mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kumekuwa na visa kadha vya mashambulizi ya gesi mwezi mmoja uliopita.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power anasema kuwa ni serikali tu ya rais Bashar al-Assad iliyo na helkopta zinazotumiwa kudondosha mapipa yenye milipuko iliyo na kemikali hatari.
Awali serikali ya Syria imekana madai hayo ikayataja kuwa propaganda.

Sunday, April 12, 2015

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA


DR. KAMALA AENDELEA KUWAVUTA WAWEKEZAJI NCHINI

Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mistra Home Shopping ya Ubeligiji. Balozi Kamala ameikaribisha kampuni hiyo kuwekeza za Tanzania.