Monday, February 25, 2013

NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA KWAWAKA MOTO

MANISPAA ya Bukoba hapakaliki, hii inafuatia hatua ya madiwani wa manispaa hiyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kususia kikao chama hicho ambacho hufanyika kabla ya kikao cha baraza la madiwani.


Baadhi ya madiwani wa CCM wamesusia kikao hicho baada ya watu wasiofahamika kusambaza waraka unaowakashfu.


Waraka huo unawakashfu madiwani kumi ambao ni pamoja na madiwani wa CCM 8 na wa vyama vya vya upinzani vinavyowaunga mkono 2.


Mwandishi wa waraka huo anatoa kashfa nzito kwa madiwani waliosaini waraka wa kutaka Mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani apigiwe kura za kutokuwa na imani naye kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabili.


Baadhi ya madiwani waliiongea walidai mgogoro ulioko kati ya Meya huyo na madiwani kuwa umeishaigawa CCM, kwa anyakati tofauti walisema kuwa hawana imani na meya huyo na ndio maana wanataka kumng'oa.


Walisema kuwa hata kama nyaraka zikisambazwa na kuwakasfu kamwe hawatarudi nyuma, "tunajua waraka huu aliyeuandaa hivyo hatuna wasiwasi nao, moto wetu uko palepale wa kumuondoa Amani madarakani" walisema bila kutaka majina yao yatakjwe.

Walisema kuwa hawataki kuongozwa na kiongozi yoyote mwenye huruka ya ufisadi ambaye anabuni miradi mingi kwa maslahi yake binafsi," Kiongozi yoyote atakayekuwa na mlengo wa kutaka kuifilisi manispaa tutakula naye sahani moja" walimaliza.


Manispaa ya Bukoba sasa kumewaka moto, pande zote zinazopingana kila mmoja anijiona ni mbabe, pande zinazopingana moja unaundwa na kundi la waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki na upande nyingine inaongozwa ana Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani.

Kambi ya Kagasheki inamtaka Meya wa manispaa ya Bukoba Amani anga'atuke na kambi ya Amani inapinga mapendekezo hayo.



No comments:

Post a Comment