Tuesday, March 03, 2015

WAJUMBE WA NEC WAHIMIZWA KUENDELEZA JUHUDU ZA KUKIIMARISHA CHAMA



NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA

Wajumbe wa halmashauri kuu  ya taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa KAGERA wamehimizwa kuendelea juhudi zao za  kukiimarisha chama hicho kwa  kubuni mikakati ya  kuleta ustawi ndani ya jamii  bila  kuwasikiliza wale wanaojaribu kuwakatisha tamaa na wakati mwingine kuwabeza.

Kauli hiyo imetolewa na katibu wa CCM wa mkoa wa KAGERA ALI AME wa hitimisho la zoezi la usambazaji wa msaada ya majaketi maalumu yatakayowawesha waendesha pikipiki kujiepusha na ajali wakati wa usiku na kutambuliwa pamoja na vifaa vya michezo.

Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi zaidi ya MILIONI SITINI na TANO umetolewa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa, NAZIR KALAMAGI na umesambaza kwa walengwa  katika vijiji TISINI na NNE vilivyoko katika kata ISHIRINI na TISA zilizoko katika wilaya ya BUKOBA vijijini.

AME amesema mambo yanayofanywa na wajumbe wa  NEC katika mkoa wa KAGERA  ya kutoa misaada mbalimbali yenye lengo la kuleta ustawi ndani ya jamii hayahusiani na masuala ya kampeni kama baadhi ya watu wanavyodhani ambao ni pamoja na mbunge wa jimbo la bukoba vijijini JASSON RWEIKIZA kwa kuwa muda wa kampeni za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi haujafika, amesema wajumbe hao wanachokifanya ni kutekeleza wajibu na kisisitiza kwa kusema kwamba hiyo kazi ya MNEC.


Kwa upande wake, YAHYA KATEME ambaye ni katibu wa jumuia ya umoja wa vijana katika mkoa wa KAGERA amesema kazi inayofanywa ya KALAMAGI  ya kukiimarisha chama inapaswa kupongezwa na kila mtu, Naye NAZIR KALAMAGI  mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa anaeleza sababu za kutoa msaada wa majaketi maalumu kwa waendesha pikipiki na vifaa vya michezo,  AMIDA KAGASHEKI  mwenyekiti wa UWT na AMIM IBRAHIMU katibu siasa uenezi na itikadi mkoani KAGERA wanaoelezaa kazi inayofanywa na MNEC huyo kwamba ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM, huku DENIS ALOYS na PETER NGEMELLA ambao ni miongoni waendesha pikipiki wakieleza msaada utakavyowanufaisha.


KALAMAGI ni miongozi mwa wajumbe wa halmashauri ambao wametekeleza wajibu wao vizuri, amekuwa wakitoa misaada mbalimbali ambayo ni pamoja uungaji mkono wa ujenzi wa vyumba vya maabara, kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya kata, hali hii inampelekea mbunge RWEIKIZA  kulalamika kwamba MNEC huyo anayafanya yote hayo kwa  lengo la kuwania nafasi ya ubunge, kauli ambayo wananchi wameitafsiri kuwa ni woga alionao kwa kuwa hakutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2010

No comments:

Post a Comment