Thursday, April 16, 2015

David Cameron akwepa mdahalo wa pili


Viongozi wa vyama vitano vya upinzani wameshiriki katika mdahalo wa pili wa moja kwa moja ulioandaliwa na BBC.
Katika hoja za kwanza, kiongozi wa chama cha Labour, Ed Miliband, amesema suala la familia za wafanyakazi atalipa kipaumbele kwanza, wakati kiongozi wa UK Independence Party,UKIP, Nigel Farage amesema atasaidia biashara ndogo ndogo. Nicola Sturgeon kiongozi wa chama cha Scotish National Party amesema anataka kuona muungano wa Uingereza unakuwa bora zaidi katika kila sehemu ya nchi hiyo. Viongozi wa Plaid Cymru na Green Party pia nao wameshiriki katika mdahalo huo.
Bwana Miliband, amesema anatarajia kupata ushindi mkubwa na hataunda serikali ya mseto na chama cha SNP.
Wagombea hao wamekuwa wakipingana katika masuala mbalimbali wakati wa mdahalo huo.
Waziri mkuu David Cameron wa chama tawala cha Conservatives na naibu waziri mkuu wake kutoka chama cha Lib Dem, Nick Clegg hawakushiriki katika mdahalo huo wa wazi.

No comments:

Post a Comment