Friday, April 10, 2015

KINARA WA MAUAJI YA KUWATAKA WATU KWA MAPANGA,KUWAONDOA MAKOROMEO NA KUWANYONYA DAMU AUWAWA NA MGANGA ANAYEWAZINDIKA MBARONI


 
NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
 
Jeshi la polisi katika mkoa wa KAGERA limeanza kufanikisha mikakati yake yenye lengo la kusambaratisha mtandao wa watu wasiojulikana wanaojihusisha na vitendo vya kufadhili na kufanya mauaji ya kuwakata kata watu kwa MAPANGA na baadae  kuwanyonya damu ambavyo  katika kata za KITENDAGULO, KIBETA na RWAMISHENYE katika manispaa ya BUKOBA.
 
Katika kusambatarisha  mtandao huo jeshi hilo  limefanikiwa  kuwaua watuhumiwa WAWILI,  JOHANES JOSEPH  ambaye ni kinara wa mauaji ya kuwakata kata MAPANGA na EDWARD THEOPHIL ambao ni miongoni mwa watuhumiwa  WANNE  walioshikiliwa kwa tuhuma ya kuhusika na  kufadhili vitendo mauaji ya kuwakata kata WATU kwa mapanga kwa  ajili ya imani za KISHIRIKINA.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA, HENRY MWAIBAMBE amesema watuhumiwa waliouwawa kwa kutumia nguvu za giza walikuwa wakijaribu kuwatoroka maofisa wa jeshi la polisi waliokuwa wakiwahoji wakati wakiwaonyesha  MAZINDIKO  wanayoyatumia katika kutekeleza mauaji, pamoja na kutoa onyo kwa wanajihusisha na vitendo hivyo pia amesema jeshi hilo kwamba linamshikilia   GAUDENSIA NDIBALEMA ambaye ni mganga wa jadi kwa tuhuma ya kuwapatia kinga wanajihusisha na vitendo vya mauaji hayo.
 

 
CLOUDS  TV imefanikiwa kuongea na baadhi ya wananchi  waliolazwa  katika  hospitali ya rufaa ya Mkoa wa KAGERA walioathrikika kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo, OMARY HABIB na ALCAD MBELWA ni miongoni mwa waathrika wa vitendo hivyo wanaoeleza walivyovamiwa na wakata mapanga hao na namna walivyojinusuru, GETRUDO RUBAKULO ni afisa muuguzi ambaye anaeleza hali ya waathirika hao, huku muuguzi mkuu wa hospitali ya rufaa BEATRICE KABUNGA  takwimu za waliofikishwa hospitalini kwa kukatwa mapanga katika kipindi cha wiki mbili.
 

 
Kufuatia vitendo vya mauaji ya kukata watu kwa mapanga katika manispaa ya BUKOBA, zaidi ya watu KUMI wameishauwawa , vitendo hivyo vinahusishwa na imani za kishirikina ambapo inadaiwa kwamba wale wanaokatwa mapanga damu zao zinavyonywa na kupelekwa pasipojulikana.
 
For more information contact +255 784 939 586/ 753 844 995

No comments:

Post a Comment