Oles Buzyna mwandishi wa habari maarufu aliyeuawa nchini Ukraine
Mwandishi maarufu wa Ukraine ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Kiev na watu waliokuwa wameficha nyuso zao.
Oles Buzyna alifahamika sana kwa maoni yake ya kuunga mkono Urusi na amefanya kazi ya uchapishaji akishirikiana na serikali ya rais Viktor Yanukovych aliyeondolewa madarakani nchini Ukraine.
Kifo chake kimekuja siku moja baada ya mwanasiasa mwenye kupendelea Urusi, Oleh Kalashnikov kuuawa katika shambulio linalofanana.
Rais Poroshenko ametaka uchunguzi ufanyike haraka, amesema mauaji haya dhidi ya watu maarufu yamefanyika makusudi na maadui wa Ukraine.