Tuesday, June 09, 2015

Kuza uwekezaji katika kawi ya Afrika kwa ajili ya ushindi mara tatu kwa watu, kawi na sayari, ripoti ya Annan inahimiza





CAPE-TOWN, South-Africa, June 5, 2015/ -- Serikali za Afrika, wawekezaji, na taasisi za kimataifa za kifedha lazima zizidishe uwekezaji wao katika kawi ili kufungua uwezo wa Afrika kama dola kuu la kiulimwengu la kiwango cha chini cha kaboni.

Huu ndio ujumbe mkuu wa ripoti mpya kutoka kwa kundi la Maendeleo ya Afrika ya Kofi Annan,  Kawi,watu, sayari :  Kutwaa nafasi za Kawi na Hali ya hewa ya Afrika. Ripoti yenyewe inatoa mwito wa kuzidishwa kwa uzalishaji wa kawi mara kumi ili kuwezesha Waafrika wote kupata umeme kufikia 2030. Hii itaondoa umaskini na ukosefu wa usawa, itaongeza ukuaji, na kuleta uongozi wa hali ya hewa ambao unakosekana katika kiwango cha kimataifa.
  
“Tunapinga kwa dhati wazo la kwamba Afrika lazima ichague baina ya ukuaji na ukuzaji wenye kiwango cha chini cha dkaboni,” alisema Kofi Annan, mwenyekiti wa kundi la maendeleo la Afrika. “Afrika yahitaji kutumia nyenzo zake zote za kawi katika kipindi kifupi kijacho, huku ikijenga misingi yenye ushindani ya miundo msingi ya kawi ya kaboni ya kiwango cha chini.”

Katika mataifa ya Afrika yaliyo chini ya Sahara, watu milioni 621 wanakosa kufikia umeme – na idadi hii inaongezeka. Pasipo kuhesabu Afrika Kusini, ambayo huzalisha nusu ya umeme wa sehemu hiyo, Afrika iliyo chini ya Sahara hutumia umeme kiasi kidogo kuliko Spain. Itamchukua Mtanzania wa kawaida wastani wa miaka minane ili kutumia kiasi sawa cha umeme na kile Mmarekani wa kawaida hutumia kwa mwezi mmoja.Na katika kipindi cha mwaka mmoja wa mtu kuchemshia birika mara mbili kwa siku nchini Uingereza hutumia umeme mara tano zaidi kuliko vile  Methiopia hutumia katika mwaka huo huo.

Ukosefu wa kawi hulemaza ukuaji wa eneo hili kwa asilimia 2-4 kwa mwaka, ikirudisha nyuma juhudi za kutengeneza nafasi za kazi na kupunguza umasikini. Kando na miaka kumi ya ukuaji, pengo la uzalishaji wa kawi baina ya Afrika na maeneo mengine linazidi kupanuka. Nijeria ni dola kuu inayouza mafuta nje ya nchi, lakini raia wake milioni 95 hutegemea kuni, makaa na nyasi kama kawi.

Ripoti yenyewe inadhihirisha kwamba nyumba zinazoishi kwa chini ya Dola $2.50 za Marekani kwa siku kwa jumla hutumia Dola bilioni $10 za Marekani kila mwaka kwa bidhaa zenye uhusiano na kawi, kama vile makaa, mafuta taa, misumaa na kurunzi. Ikipimwa kwa misingi ya kwa-kiasi , nyumba masikini zaidi za Afrika hutumia yapata Dola za Marekani $10/kWh kwa mwangaza mara 20 zaidi ya nyumba tajiri za Afrika. Kwa kulinganisha, gharama ya wastani ya kitaifa ya umeme inchini Marekani ni Dola za Marekani $0.12/kWh na Uingereza ni Dola za Marekani $0.15/kWh. Huu ni mwanguko wa kiwango fulani cha soko.

Teknolojia za ufanywaji upya wa gharama za chini zinaweza kupunguza gharama za kawi, ikifaidi mamilioni ya nyumba masikini, kuleta nafasi za uwekezaji, na kupunguza uchafu wa kaboni.

Ripoti yenyewe inasema viongozi wa Afrika lazima waanzishe mageuzi ya kawi ambayo yataunganisha wale hawajaunganishwa, na inayoshughulikia mahitaji ya watumizi, biashara, na wawekezaji kwa ajili ya umeme wa gharama ya chini na unaoweza kutegemewa.

Ripoti hiyo ya Maendeleo ya Afrika ya 2015 inahimiza serikali za Afrika :

•          Kutumia gesi ya asili ya eneo hilo kutengeneza kawi ya kutumika nyumbani na pia kuuza nje ya nchi, huku ikikusanya uwezo mkubwa wa kawi yenye kufanywa upya ya Afrika ambayo haijatumika.

•          Kusitisha ufisadi, kufanya usimamizi wa huduma kuwa wazi zaidi, kuimarisha sheria, na kuongeza bajeti ya miundo msingi ya kawi.

•          Kuelekeza upya zile Dola bilioni $21 za Marekani zinazotumika kufidia huduma zinazopata hasara na matumizi ya umeme– ambazo hufaidi haswa matajiri – kuelekea fidia za uunganishwaji na uwekezaji wa kawi yenye kufanywa upya ambayo huleta kawi kwa masikini.

Ripoti hii inaomba kuimarishwa kwa uhusiano wa kimataifa kufunga pengo la ufadhili wa sekta ya kawi ya Afrika, yenye kukadiriwa kuwa Dola bilioni $55 za Marekani kwa mwaka hadi 2030, ambalo linajumuisha  Dola bilioni $35 za Marekani za uwekezaji wa viwanda, upeperushaji na usambazaji, na Dola bilioni $20 za Marekani kwa gharama za ufikiaji kwa wote.

Hazina ya kiulimwengu ya uunganishaji yenye lengo la kuwafikia Waafrika milioni 600 zaidi kufikia 2030 inahitajika kuendeleza uwekezaji ndani na nje ya mfumo wa ugavi wa kawi.

Wenye kutoa msaada na taasisi za kifedha zinafaa kufanya kazi zaidi ili kufungulia uwekezaji wa kibinafsi kupitia kwa dhamana na fedha za kushughulikia madai.

No comments:

Post a Comment