Sunday, August 02, 2015

BALOZI KAMALA, PROFESA TIBAIJUKA, CHARLES MWIJAGE KIDEDEA, KARAMAGI AANGUKIA PUA



MAKADA wa wanaotarajiwa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika  Kaagera kwenye nafasi yaubunge wamepatikana, katika uchaguzi wa kura za maoni za chama, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na jumuia ya ulaya, Diodorus Kamala ameibuka mshindi katika kura za maoni za jimbo la Nkenge.

Dkt. Kamala ameibika mshindi baada ya kuwabwaga kwa kura nyingi makada watano aliokuwa akichuana nao ambao  ni pamoja na Asumpta Mshama aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, katika jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ameibuka mshindi baada ya kumshinda mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Muleba Mhaji Bushako.

Katika mkoa wa Kagera makada wa CCM wengine walioibuka na ushindi ni pamoja na Jassn Rweikiza aliyembwaga Nazir kalamagi, swahiba mkubwa wa Edward Lowassa aliyeamia CHADEMA hizi karibuni, Muleba kaskazini, naibu waziri wa Nishati na Madini, Bw. Mwijage amekuwa mshindi.

Jimbo la Biharamulo Oscar Mkassa , mbunge wa zamani wa jimbo hilo ameibuka mshindi baada ya kuwashinda aliokuwa akichuana nao ambao ni pamoja na Anatory Choya, katika jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki ndiye ameibuka mshindi.

Hatima ya walishinda  katika kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni itategemea maamuzi ya vikao vya juu ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment