Sunday, August 02, 2015

Kampuni ya Business Connexion yahamasisha kuhusu fursa zilizopo



 
DAR ES SALAAM, Tanzania, July 28, 2015/ -- Tanzania ina fursa nyingi ambazo bado hazijatumika. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi unategemewa kukua kwa wastani wa asilimia7.2 mwaka huu na uwekezaji wa serikali kwa kiasi kikubwa katika mkongo wa taifa unaongeza biashara na upatikanaji wa teknolojia kwa raia ili kujenga fursa za kusonga mbele kwenye teknolojia zetu. Pamoja na kuibuka kwa teknolojia nyingi zisizokuwa na mpangilio, hatua hii imewekwa kwa ajili ya kuongezeka kwa fursa nyingi. Haya ni maoni ya Jane Canny, Afisa Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion.
 
Kampuni ya business Connexion Tanzania imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 2000,lengo lake kubwa hasa ni kujikita katika huduma za kifedha, mawasiliano ya simu, nishati na madini na sekta ya umma. Kupitia matumizi bunifu ya teknolojia na ushirikiano wetu na UmojaSwitch Consortium, Tunatoa huduma ya upatikanaji wa miundombinu ya malipo iliyo salama katika benki 28 na mashine za ATM 200 nchini Tanzania. Miundombinu hii imeunganishwa na swichi tano za malipo ndani ya Afrika Mashariki ili kuruhusu miamala ya kimataifa, makampuni makubwa matatu ya mitandao ya simu ili kuwezesha malipo ya simu na taasisi mbalimbali za serikali katika kuwezesha makusanyo ya malipo ya kielektroniki.
 
Muunganiko wa vitu hivi vinavyotengeneza mtandao unabadili namna ya uendeshaji wa biashara kwa kasi kubwa," anasema Canny. "Kama wateja watakuwa wameunganishwa zaidi, mahitaji yao yanabadilika na mashirika kwani yanapaswa kubadilika kama teknolojia na namna tunavyoitumia inabadilika, au wanakutana na kile kilichoachwa nyuma na washindani wao.
 
Anaongeza kuwa, pia kuna miradi kadhaa inayoendelea ya kuunganisha Manispaa na hospitali nchini kote ili kuwezesha makusanyo ya malipo ya kielektroniki. ”Huu ni mfano mkubwa ambapo teknolojia imekuwa ikitumiwa kufanya maisha ya watumiaji yawe rahisi zaidi," anasema Canny. "Na kama teknolojia inaendelea kukua, ndivyo jinsi ambavyo wateja wataingiliana na watoa huduma wao. Kwa mfano,Katika miaka mitano ijayo kitengo cha mawasiliano cha karibu au kitengo cha teknolojia cha mawasiliano kilicho karibu kitatumika nchini kote ili kuwezesha malipo ya rejareja kupitia simu ya mkononi. Pia tunatengeneza kiunga muhimu cha kwenye simu kinachohusiana na benki katika intaneti, ambacho kitakuwa kinaratibiwa katika kituo chetu cha data hapa nchini.
 
Canny anasema muungano uliopendekezwa na Telkom hautarajiwi kuwa na athari yoyote juu ya uendeshaji nchini na kampuni bado linabaki likijikita katika soko la Tanzania. Bila kujali matokeo ya muungano uliopendekezwa, ni biashara kama kawaida kwetu. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kutoa suluhisho zenye ubunifu kwa wateja wetu. Tutaendelea kuwekeza katika miundombinu ya huduma za ubadilishaji wa kifedha ili kulinda nafasi yetu katika soko la huduma za kifedha, "anasema. "Kituo chetu cha data nchini,ambacho kinaratibu moja ya suluhisho kubwa za makampuni ya mawasiliano ya simu, na huduma za kufufua data pia zinaendelea kukua.
 
Canny anaamini muungano huu uliopendekezwa unaenda sambamba na mwenendo wa kimataifa ambapo kampuni za  mawasiliano ya simu na huduma za TEHAMA zinaungana. Inatuwezesha kuinua miundombinu ya mawasiliano ya Telkom na kutoa ufumbuzi kwa wateja wetu unaokuwa na mwisho. Wakati Telkom haijaanza uendeshaji wake nchini Tanzania, kwa sasa unasehemu kidogo nchini. Hii ni pamoja na mkakati wao wa ushirikiano wa kuunganisha na uwekezaji wa miundombinu ya mawasiliano chini ya bahari kote Afrika, bila shaka kutafaidisha wateja wetu, "anahitimisha.
 

No comments:

Post a Comment