Wednesday, April 29, 2015

PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA BRITISH AMERICAN TOBACCO

  PRIME MINISTER MIZENGO PINDA SPEAKING TO BRITISH AMERICAN TOBACCO OFFICIALS IN HIS OFFICE, DAR ES SALAAM, APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS  JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA, ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA (PMO PHOTO)

PRIME MINISTER, MIZENGO PINDA POSES FOR A GROUP PHOTO WITH BRITISH AMETICAN TOBACCO OFFICIALS AT HIS OFFICE IN DAR ES SALAAM ON APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA- BAT AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA, PM, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO AND TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA. (PMO PHOTO)

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA BRAZILI



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz na kujadiliana mambo kadhaa kuhusu maendeleo na mahusiano baina ya nchi hizo mbili.



Akizungumza na Balozi Luz ofisini Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015), Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano ambao ameutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka sita ambacho amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.



Balozi Luz ambaye amepangiwa kwenda Jordan kwenye kituo kipya, alisema anaondoka nchini akiamini kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea mambo aliyoyaanzisha ikiwemo mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao la pamba kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.



Balozi Luz ambaye alifika kumuaga Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili kusomea kozi za Uzamili (Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.



“Wanafunzi hawa wawili waliondoka Februari mwaka huu, ni kati ya wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine watano walikosa ufadhili kutoka kwenye taasisi zao. Mmoja anasomea Geo-Physics na mwingine Oil Engineering,” alisema Balozi Luz.



Balozi Luz ambaye anatarajia kuondoka nchini mapema mwezi ujao, amepangiwa kituo kingine ambapo ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.







IMETOLEWA NA

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

S.  L. P. 3021,







RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kisha kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.
rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini  kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinto Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).

RAIS KIKWETE AZINDUA MELI VITA MBILI ZA KIKOSI CHA WANAMAJI CHA JWTZ

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa amri kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
Add caption
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015

BALOZI KAMALA ASHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA BIASHARA UBELIGIJI


Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali baada ya Ufunguzi wa Kongamano la Biashara la Kimataifa linalofanyika Ubeligiji. Balozi Kamala anaongoza ujumbe wa Wafanyabishara zaidi ya hamsini kutoka Tanzania na maofisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wanaoshiriki katika Kongamano hilo.

Monday, April 27, 2015

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU HASHIM MBITA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji 
familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. 
Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro, 
baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha 
maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro, 
baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma kikwete wakimsikiliza mtoto wa Marehemu Bw. Iddi Mbita kuhusu taratibu za mazishi walipokwenda kuifariji familia ya 
Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. 
Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro, 
baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.

Rais Kikwete akiondoka msibani

Picha na IKULU

SERIKALI KUIIMARISHA OFISI YA TAKWIMU – WAZIRI MKUU




WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imedhamiria kuiimarisha Ofisi ya Takwimu ya Taifa ili iweze kutoa huduma bora siyo tu kwa Serikali bali hata kwa wananchi kwa sababu wana haki ya kupatiwa takwimu sahihi.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Aprili 27, 2015) wakati akifungua kongamano la siku tatu kuhusu Uongozi na Usimamizi wa Mifumo ya Takwimu liliondaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (International Statistical Institute – ISI) kwenye hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wakuu wa taasisi za takwimu barani Afrika wanaoshiriki mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Kongamano hilo limekusanya washiriki zaidi ya 50 kutoka nchi 31 za Afrika zinazozungumza Kiingereza kwa nia moja ya kuweka msukumo kwenye umuhimu wa matumizi ya takwimu katika kuleta maendeleo ya nchi husika.

“Kama nchi, Tanzania tunakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa takwimu lakini tumeanza kulitazama jambo hili na ndiyo maana nimesema Serikali imedhamiria kuiwezesha taasisi hii ya takwimu ili itoe takwimu sahihi kwa Serikali kwa upande mmoja na kwa wananchi kwa upande mwingine…wao ni wadau wakuu wa takwimu hizi,” alisema Waziri Mkuu.

“Tuna lengo la kuifanya taasisi hii iwe na hadhi ya kimataifa katika kutoa takwimu zake. Sote tunatambua kwamba ulimwengu wa sasa ni wa kidigitali, na bila kuwekeza kwenye hilo hatuwezi kufika mbali,” alisema.

Aliwataka wakuu wa taasisi za takwimu barani Afrika waangalie uwezekano wa kufanya kazi kwa karibu pamoja Halmashauri za miji na wilaya kwani huko ndiko kwenye rasilmali kubwa ya takwimu na ndiko maendeleo ya wananchi yaliko.

“Ukichukua mfano wa Tanzania, tuna Halmashauri za Wilaya na Miji zaidi ya 160. Mkiamua kufanya kazi kwa karibu na Serikali za Mitaa mtapata takwimu za ajabu kwani huko ndiko kwenye miradi yote ya maendeleo. Tukumbuke kuwa asilimia 75 hadi 80 ya Watanzania wote wanaishi vijijini,” alisema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua kongamano hilo, Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema takwimu ni mali ya umma na hazipaswi kutolewa kwa upendeleo.
Waziri Ghasia ambaye alizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Bibi Saada Mkuya, alisema takwimu zenye ubora na ubunifu ni muhimu sana kwa ajili ya kupanga kazi za maendeleo ya Taifa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Dk. Albina Chuwa alisema kuna haja ya Serikali za nchi za Afrika kuweka kipaumbele kwenye suala la upatikanaji wa takwimu na lisiwe suala la kuchukuliwa kijuujuu tu, bali lichukuliwe kama sekta kamili ya kipaumbele.

“Naziomba nchi za Afrika zianze kuchukulia takwimu kama sekta ya kipaumbele kwenye mipango yao ya maendeleo ya Taifa… tunapokaribia kuhitimisha muda wa kutekeleza malengo ya milenia (MDGs), tunapaswa kujielekeza kwenye viashiria vipya zaidi ya 300 ambavyo vimeainishwa, hivi viko kwenye ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa”.

“Katika bara la Afrika, kama hatutaamua kuainisha viashiria vyetu wenyewe kuanzia ngazi ya Kitaifa, wataibuka watu na kututengenezea viashiria ambavyo havina uhalisia kwa sababu hawajui matatizo ambayo bara la Afrika linakumbana nayo,” alisema Dk. Chuwa.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

Warundi 152,572 wawa raia wa Tanzania




Waliokuwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania zaidi ya 152,572 walioingia nchini humo tangu mwaka 1972, wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania na kuwa huru kuishi kama Watanzania wengine.
Wakimbizi hao walikuwa wameomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na waziri wa mambo ya ndani mwaka 2010, sasa ni halali kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za udiwani na ubunge.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa vyeti hivyo, mkuu wa makazi ya Mishamo, Frederick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka 2014 katika makazi ya Katumba mkoani Katavi magharibi mwa Tanzania ambako watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye kuhamia katika makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania ambako wakimbizi 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo.
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Isaack Nantanga amesema hatua ya Tanzania kuwapa uraia wakimbizi hao ni kutokana na hiyari yao na kwamba serikali ya Tanzania ilishauriana na Burundi na hatimaye kukubaliana wapatiwe uraia wanaotaka wa kuwa Watanzania.
Hata hivyo si mara ya kwanza kwaTanzaniakutoa uraia kwa wakimbizi wanaoishi Tanzania kwa muda mrefu. Tanzania imefanya hivyo kwa wakimbizi wa Burundi na Somalia ambao wameishi Tanzania kwa miaka mingi.

Maandamano:Jeshi lasambazwa Burundi

Jeshi la Burundi limetawanywa nchini humo kujaribu kukabiliana na wale wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu.
Polisi walivunja maandamano ya Wanaharakati na wapinzani nchini humo waliongia mitaani kwa siku ya pili kufanya maandamano.
Waandamanaji kadha walipigwa risasi jana Jumapili na watu wanne wanaripotiwa kufariki




Sunday, April 26, 2015

Tigo launches bid to become biggest 4G network in Tanzania


 
Tigo new 4G technology makes Tigo the fastest Internet network in the country
 
DAR ES SALAAM, Tanzania, April 24, 2015/ -- TIGO Tanzania (http://www.tigo.co.tz) has today launched a brand new 4G LTE technology that will make it the biggest and fastest Internet network in the country.
 
 
Speaking at the launch, Tigo Interim General Manager Cecile Tiano said: “This once again demonstrates our company’s commitment to the digital lifestyle transformation and its leadership in delivering cutting edge technology and innovation in this market.”
 
The 4G LTE network means faster speeds to surf and download content from the Internet and make Skype calls. It also significantly enhances the customer experience for video streaming or conferencing. The new technology is about 5 times faster than the 3G technology currently available in the market.
 
The 4G LTE technology is a standard for wireless communication of high-speed data. It has the capacity to efficiently transfer large amounts of data at an unparalleled speed. It can also accommodate more applications such as video conferencing, high definition content, video blogs, interactive games and video downloads on social networking sites. 
 
With the surging use of smartphones among the Tanzania population, 4G technology will enable Tigo customers to enjoy a world class experience of increased speed and quality of internet access through the network.
 
“Today’s launch covers Masaki and Mlimani City areas within Dar es Salaam but our plan is to fully cover the city by end of July, ensuring quality coverage in Kinondoni, Ilala and Temeke in places such as Upanga, Posta, Tegeta, Mbagala, Tabata, Kimara, Mbezi, Ukonga, Salasala, Mikocheni, Msasani, Sinza and so on,” Ms Tiano explained.
 
“We will also launch 4G in Arusha, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza and Tanga by end of August. This will make us by far the biggest 4G network in Tanzania,” she added.
 
The 4G technology launch is part of Tigo’s commitment to continue improving the quality and coverage of its network and bring world class products and services to Tanzanians.
 
Tigo recently announced plans to invest US $120 million in 2015 on its network expansion and improvement. The investment includes scaling up its 3G sites and fibre network countrywide to make the internet accessible to more users.
 
FACT BOX:
 
•          Tigo new 4G technology makes Tigo the fastest Internet network in the country
•          The company is investing $ 120 million on network improvement and expansion in 2015
•          Network has 8.5million total subscribers
•          4G will increase internet speed by 5 times from the current 3G technology
•          4G launch covers Masaki, Mlimani city areas in Dar
•          4G to cover whole city and six regional capitals by August 2015
 
About Tigo:
Tigo Tanzania (http://www.tigo.co.tz) is the leading innovative telecommunication company in the country, distinguished as a fully-fledged digital lifestyle brand. Offering a diverse product portfolio in voice, SMS, high-speed internet and mobile financial services, Tigo has pioneered innovations such as Facebook in Kiswahili, Tigo Pesa App for Android & iOS users, and East Africa’s first cross-border mobile money transfer with currency conversion. 
 
The Tigo 3G network guarantees the best services to its subscriber’s in all regions across the country.  Between 2013 and 2014 alone the company launched over 500 new network sites and plans to double its investment by 2017 in terms of coverage and additional capacity networks for deeper penetration in rural areas. With over 8.5 million registered subscribers to their network, Tigo directly and indirectly employs over 100,000 Tanzanians including an extended network of customer service representatives, mobile money merchants, sales agents and distributors.
 
Tigo is the biggest commercial brand of Millicom, an international company developing the digital lifestyle in 44 countries with commercial operations in Africa and Latin America and corporate offices in Europe and the USA. With the certain knowledge that only constant innovation will keep them on top, Millicom keeps creating greater shareholder value; applying their concept of “demand more” is how they do business and retain their position as digital lifestyle leaders in some of the most unique and challenging markets.
 
SOURCE 
Tigo Tanzania

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA MKUU WA WILAYA YA KYELWA


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji Mama Francisca Kitenga baada ya mazishi ya mumewe, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola , Morogoro mjin.i
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telesphor Mkude baada ya mazishi ya  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na  baadhi ya Wakuu wa Wilaya walioshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, , marehemu,Luteni Kanali Benedict Kitenga  yaliyofanyika kwenye makaburi ya  Kola , Morogoro mjini.

Wednesday, April 22, 2015

Jeshi laapa kuwashinda Boko Haram

 


Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa linafanya oparesheni ya mwisho kwenye msitu moja ambao unaaminiwa kuwa ngome kuu ya wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi (Chris Olukolade) alithibitisha kuwa opaesheni zinaendelea kwenye msitu wa Sambisa karibu na mpaka na Cameroon.
Serikali ya Nigeria inasema kuwa Boko Haram wako mbioni na jeshi limeapa kuwashinda kabla ya kuapishwa kwa rais mpya Muhammadu Buhari tarehe 29 mwezi Mei.
Inaaminika kuwa zaidi ya wasichana 200 wa shule ambao walitekwa nyara mwaka mmoja uliopita kutoka mji wa Chibok huenda wameshikiliwa ndani ya msitu huo

Hali yaelezwa kuwa mbaya zaidi Yemen

 

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini Yemen, huku Mji mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha siku tisa zilizopita.
Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini humo Robert Mardini amesema ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa alipotembelea mji wa Aden, na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni upelekaji wa huduma za kitabibu.
Awali Saudi Arabia ilisema itaendelea kutumia jeshi kuzuia waasi wa kihudhi kudhibiti Yemen, waasi nao wametaka kumalizwa kwa mashambulizi ya anga dhidi yao na kuanza mazungumzo.
Mpiganaji anayemuunga mkono Rais Abdrabbuh Mansour Hadi amesema ni mapema mno kuanza kuzungumzia makubaliano kati ya pande mbili.

PINDA AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA BARAZA LA BIASHARA LA CHINA

 WAziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara  la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha  Tanzania - China Promotion Centre, Bw. Xian Ding. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara  la China na Afrika ( Vice Chairman of China Africa Business Council, Bw. Huarong Zhang kabla ya mazungumzo yao Ofisini  kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,Aprili 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MKUU WA WILAYA YA KYERWA MAREHEMU LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) LEO HOSPITALI KUU YA JESHI YA LUGALO, DAR ES SALAAM

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrishi Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (Mstaafu) aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ambaye alifariki jana asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho huko Morogoro.
 Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (Mstaafu) aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ambaye alifariki jana asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho huko Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrishi Kikwete akifariji mjane wa marehemu baada ya kutoa heshima  zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (Mstaafu) aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ambaye alifariki jana asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho huko Morogoro.

Tuesday, April 21, 2015

WATANZANIA WALIOKO NJE WASHAURIWA KUHAMISHA MITAJI YAO KWA KUWEKEZA NCHINI, PASKAZIA BALONGO ANASIMULIA



NA AUDAX MUTIGANZI, BUKOBA +255 784 935 586

Uwekezaji  katika nchi hii ni sera iliyotiliwa mkazo na rais wa jamhuri ya muungani wa Tanzania wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa, sera hii imechangia kuchochea kasi ya maendeleo kwa kuleta mabadiliko katika  nyanja za  kijamii na kiuchumi.

Ninachotaka kusema  sera ya uwekezaji imechangia kuboresha na kuimarisha huduma katika Nyanja mbalimbali ndani ya jamii, imeongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani, imekuza  sekta ya utalii, imeboresha masuala ya kilimo mambo ambayo yanachangia ukuaji wa pato la taifa.

Ni lazima tukubali kwamba sera hii imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ukosefu wa ajira hasa kwa wanaohitimu masomo yao katika ngazi mbalimbali hapa nchini walikokuwa wakitegemea sana ajira zinazotolewa na serikali ambazo ni chache  ukilinganisha na idadi ya wanafunzi wanaohitimu masomo yao katika vyuo  vya elimu ya juu na elimu ya kati.

Kwa  maana hiyo hatuna budi kumpongeza rais mstaafu wa awamu ya tatu, kwa kutilia  mkazo  suala la uwekezaji, katika kutilia mkazo suala la uwekezaji  aliweka mazingira mazuri  ambayo hadi sasa yanaendelea kuwavutia wale wanaojitokeza kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali.

Ndugu zangu Watanzania  ni lazima tukubali kwamba mchango wa Rais Mstaafu Mkapa katika kuendeleza nchi hii ni  mkubwa,  sera ya uwekezaji imechangia kwa kiasi kikubwa matumizi ya rasilimali zilizo adimu zinazopatikana  hapa nchini ambazo  ni pamoja na malighafi zinazotumiwa na viwanda vya wawekezaji vilivyoko hapa nchini vinavyozalisha bidhaa mbalimbali.

Ni kweli sera hii ni nzuri imechangia kuchochea kasi ya maendeleo, katika utafiti wangu nilichokigundua ni kwamba wawekezaji  walio wengi wanaojitokeza kuwekeza hapa nchini ni wale wanaotoka nje ya nchi.

Kwa uelewa nilikuwa nao ni wawekezaji wachache toka nje ya nchi ambao wanaweza kuwa na machungu ya nchi hii katika kuhakikisha  inapiga hatua kubwa kimaendeleo.
 Ninachokielewa kila mwekezaji anayejitiokeza kuwekeza hapa nchini lengo lake kubwa ni kuchuma mali na kuondoka bila kutangulizambele maslahi ya nchi, hakuna mwekezaji ambaye anaweza kuwa na machungu ya nchi hii bila kutanguliza maslahi yake binafsi kwa kuwa anawekeza kwa lengo la kupanua myaji wake ndio maana wawekezaji wanajitokeza wanakuja kibiashara zaidi.

Je, sisi Watanzania wenye uwezo tulioko ndani na nje ya nchi tuko wapi? Ni lazima tujiulize swali hilo kwa kuwa ni la ufahamu, kinachonishangaza na kuniuma ni pale ninapowaona baadhi ya Watanzania wenye mitaji mikubwa  wakosa moyo wa uzalendo hasa pale wanapofikia  katika mataifa mengine.

Kuna usemi ‘usemao samaki mmoja akioza sio kwamba wote wameoza’  usemi huu nitakubaliana nao sio kwamba watanzania wote waishio nje ya nchi wenye mitaji mikubwa wanaokosa moyo wa uzalendo, kuna baadhi ya Watanzania  wanaokumbuka walikotoka  kwa kutenga mitaji walionayo kwa kuwekeza hapa nchini.

Miongoni mwa Watanzania waliotenga sehemu ya mitaji waliyo na hatimaye kuwekeza nchini ni pamoja na Paskazia Barongo Mtanzania aishiye nchini Sweeden ambaye amejitokeza na kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kuanzisha chuo cha ualimu kinachojulikana kwa jina la ERA kilichoko katika mtaa wa Kagemu ulioko katika kata ya Kitendagulo, mkoani Kagera.

Chuo hicho kinatoa mafunzo ya ualimu daraja la tatu ngazi ya cheti, Bi Balongo anasema  kwamba chuo hicho kimeanza rasmi kutoa mafunzo ya ualimu kuanzia mwaka jana mwezi wa nane, anaeleza kwamba  alifikiria mpango wa kuanzisha chuo hicho  mwaka 2008 baada ya kupona katika ajali mbaya sana ya gari aliyoipata akiwa nchini Sweeden.

Anaeleza kwamba baada ya kupona katika ajali hiyo alijisikia kwamba ana deni kubwa kwa watanzania hususani wazaliwa wa mkoa wa Kagera hasa waliomuombea hadi akafikia hatua ya kupona, anasema kuwa katika ajali alivunjika vunjika sehemu mbalimbali za viungo vya  mwili wake.

Bi. Barongo anasema katika kuwaenzi Watanzania walimuombea hadi akapona baada ya ajali hiyo alilazimika kuwekeza katika sekta ya elimu na sekta ya afya, anasema amelazimika kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuwa inamchango mkubwa katika ustawi ndani ya jamii.

Anasema kuwa anachokiamini ni  kwamba kama waliompatia matibabu hadi akapona  wasingekuwa na elimu wasingefanya chochote kulingana na hali mbaya aliyokuwa nayo baada ya kupata ajali hiyo, anaendelea kusema kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha pamoja na kukabiliwa na changamoto nyingi.

Anabainisha kwamba hakulazimika kuwekeza katika sekta ya elimu kwa lengo la kufanya biashara bali amewekeza katika sekta hiyo kwa lengo la kutoa huduma, katika kutoa huduma anasema kwamba chuo chake kinampokea mwanafunzi yoyote aliyemaliza kidato cha nne bila kujali ufaulu wake.

Bi. Balongo anasema wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne wenye ufaulu mzuri  wanajiunga moja kwa moja na mafunzo  ya cheti cha ualimu ngazi ya daraja la tatu na wale wanaojiunga na chuo hicho wenye ufaulu usioridhisha wanapatiwa elimu maalumu ya kuwawezesha kurudia mitihani yao inayowapa sifa ya kufanya mitihani ya cheti cha ualimu.

Anaendelea kusema kuwa chuo chake kinatoa elimu ya kiwango cha juu ambayo inaenda sambamba na vyuo vya ualimu vinavyomilikiwa na serikali, anasema kuwa ataendelea kukiboresha chuo hicho , anasema kuanzia mwaka kesho chuo hicho kitaanza kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya kilimo.

Bi. Barongo anasema  chuo kimelazimika kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya kilimo kwa lengo la kuwawezesha vijana waweze kujiari wenyewe  na ili waachane na dhana ya kutegemea ajira chache zinazotolewa na serikali.

Amesema  mafunzo yatakayotolewa kwa vijana yatawawezesha kujifunza mbinu bora za kilimo, anabainisha kuwa kilimo kinalipa vizuri ukilinganisha na shughuli nyingine za uzalishaji mali zinazohitaji mitaji mikubwa.

“ Nina mpango mkubwa wenye lengo la kuboresha maisha ya vijana, mimi sikuwekeza kwa leng la kupata faida nimewekeza katika sekta ya elimu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi na ndio maana najitolea katika mambo mengi, mimi ni tofauti na wawekezaji wengine wanaotafuta faida” anasema.

Bi.Barongo anasena chuo chake cha ERA kina eneo kubwa ambalo litawawezesha wanafunzi watakaojitokeza kusoma masuala ya kilimo kujifunza kwa vitendo badala ya kupata mafunzo ya masuala ya kilimo kwa njia ya vitabu.

Anasema chuo kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 129 na matarajio ya chuo hicho ni kupokea   wanafunzi 500 kwa wakati mmoja pindi miundo mbinu itakapokamilika, akielezea miundo mbinu ya chuo anasema kwa sasa chuo hicho kina jumla ya mabweni mawili ya wasichana na moja la wavulana.

Akielezea miundo mbinu mingine katika chuo hicho anasema kina madarasa matatu , chumba cha walimu, maktaba dogo, chumba cha komputa, ofisi ya walimu, ofisi ya mkurugenzi na ofisi ya makamu mkuu wa shule na jiko la kisasa, anaongeza kuwa chuo hicho kwa sasa kinatoa ajira kwa watu 26.

Katika kueleza changamoto mbalimbali zinazokikabili utendaji wa kazi wa chuo hicho Bi.Barongo anasema utaratibu wa serikali kubadili mifumo yake mara kwa mara kwamba inaathiri kiwango cha elimu.

Akitoa ufafanuzi wa changamoto hiyo  anaeleza kwamba chuo hicho kwa mara ya kwanza kilisajiliwa na wizara ya elimu, anasema kwa sasa vyuo vyote binafsi vinatakiwa kusajiliwa NACTE,  anaendelea kusema kuwa ubadilishwaji wa mfumo wa usajili wa vyuo kwamba unavigharimu na unawavunja moyo wawekezaji katika sekta ya elimu.

Ameishauri serikali  kuboresha zaidi  manzingira ya uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha inazishawishi taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wawezekazi katika sekta ya elimu yenye riba na masharti nafuu, tofauti riba inayotozwa kwa wawekezaji katika sekta nyingine zinazojihusisha na masuala ya biashara ya moja kwa moja.

Pia ameishauri serikali kuondoa ukilitimba katika zoezi la usajili wa  mashule na vyuo vya elimu kwa kuwapa madiwani wa manispaa, majiji na halmashauri za wilaya madaraka makubwa ya kutoa vibali vya uanzishwaji wa mashule na vyuo.

Bi.Barongo anasema kwa kiasi Fulani mgogoro katika manispaa ya Bukoba ambao ulipelekea kutofanyika kwa vikao vya baraza la madiwani  kwamba ulimuathiri sana kwa kuwa ulimchelewesha upatikanaji wa kibali cha kuanzisha chuo hicho hali iliyomgharimu sana kwa kuwa alikuwa analazimika kuja nchini mara kwa mara kufuatilia usajili.

Anamalizia kwa kuwapongeza wale wote waliomtia moyo hadi akatimiza adhima yake ya ya kuanzisha chuo cha ualimu, pia amewahimiza Watanzania kukumbuka walikotoka  kwa kutenga mitaji waliyonayo na kuwekeza hapa nchini kwa kuwa Watanzania ndio wenye uchungu na nchi yao.

Sunday, April 19, 2015

Suluhu yatakiwa haraka kuhusu wahamiaji


Boti ya Italia iliyokuwa katika Operesheni ya kuokoa wahamiaji ikiwa imebeba wahamiaji walikuwa wakisafiri kwenda Ulaya
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi ametoa wito wa kufanyika kikao cha dharura cha viongozi wa umoja wa ulaya kujadili swala la wahamiaji wanaoangamia kwenye bahari ya Meditarenean wakijaribu kuingia ulaya. Inafuatia ajali ya hivi punde ambao karibu watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya boti kuzama baharini kaskazini mwa Libya, kilomita 200 kutoka kisiwa cha Lampedusa, nchini Italia.
Manusura 28 wa janga la hivi punde kwenye bahari ya Meditaranean walitarajiwa kufikishwa kisiwani Sicily alfajiri ya Jumatatu. Hadi kufikia usiku, ni miili 24 iliyokuwa imeopolewa, na maafisa wa usalama kwenye pwani ya Italia, wakaipeleka kisiwani Malta.
Ni vigumu kuhakikisha idadi ya watu walioanza safari kwenye boti hiyo kutoka pwani ya Libya. Lakini walionusurika wanasema walikuwa kati ya watu 500 na 700 kabla ya kupinduka kilomita mia mbili kutoka Lampedusa, kwenye maji ya Libya.
Ikiwa idadi hiyo itathibitishwa basi hii itakuwa ndio ajali mbaya zaidi kati ya nyingi ambazo zimekuwa zikitokea karibuni kwenye bahari ya mediteranean, huku watu wakifanya safari za hatari kutafuta maisha bora ulaya.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi amesema zaidi ya mawakala 900 wa kusafirisha watu wamekamatwa. Alisema suluhu la tatizo la wahamiaji si kutafuta manusura baharini, bali kuwakabili mawakala hao wa kusafirisha watu, akiwaita wafanyabiashara wa watumwa wa leo. Ametaka kikao cha umoja wa ulaya ndani ya wiki moja kujadili tatizo hili kubwa.
Papa Francis kwenye misa ya Jumapili alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua ya haraka kuepuka janga lingine kama hilo.
Meli pamoja na helikopta za Italia na Malta ziliendelea na shughuli ya kusaka miili usiku kucha. Mamlaka za Sicily zinasema wengi wa abiria kwenye boti iliyozama walikuwa ni kutoka mataifa ya Algeria, Misri Somalia, Senegal na hata Zambia.

Kwanini wanaume wanajitoa uhai ? Soma utafiti



Utafiti umeonesha kuwa wanaume wenye umri kati ya 40-50 wamo katika hatari kubwa ya kujinyonga
Wanaume wengi wenye umri kati ya miaka arobaini na 50 wamo katika hatari kubwa ya kujiua kuliko wanawake.
Kijana mmoja kutoka Uingereza ,Simon Jack alifanya utafiti huo baada ya baba yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na umri wa miaka 44.
Jack anasema alianza kuwa mdadisi kwa simulizi zote au habari kuhusu watu wanaojiua na amegundua kuwa wote ni wanaume.
Wanaume wanazongwa na mawazo na hawana wa kusema naye
''Sikujua kuwa kujiua ni adui mkubwa wa watu wenye umri chini ya miaka 50,ila sasa nafahamu kwanini wanaume mia moja wamejiua ndani ya wiki''.
Idadi hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko wakati wowote katika miaka 14 iliyopita ya wanaume wanaomaliza maisha yao wenyewe ni mara nne ya wanawake.
Jack,alitamani kufahamu sababu inayowafanya wanaume kufanya matukio hayo zaidi.
Na kama kuna namna yeyote ya kuzuia mauaji haya, ''Nilijiuliza nini kinachopelekea wanaume hawa kufanya hivi?
''Miaka 40 ni miaka ambayo mtu ana majukumu mengi, Unaweza kudhani kuwa mke wake amemuacha na kuchukua watoto wote,au kapoteza kazi yake katika umri huo wakati ni vigumu kupata mwingine''alihoji Jack.
''Au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake''.
Kwa upande wa baba yake Jack, haikuwa hivyo kwani alikuwa ni baba mzuri mwenye upendo kwa familia yake,mwenye uwezo nau maarufu.
Kila mtu atakubali kuwa ni tatizo kubwa katika familia pale unapompoteza mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha uliokithiri au kuachwa na mpendwa wako.
Wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika maisha.
Prof Rory O'Connor ambaye anaongoza kituo maarufu duniani cha utafiti katika chuo kikuu cha Glasgow,
anasema tabia ya kujuiua ni tatizo la kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.
Ingawa watu wenye matatizo ya akili uwa ni vigumu sana kujiua ni asilimia tano tu ndio wanaweza kujiua kutokana na upungufu wa akili.
Hata hivyo katika maamuzi kuna tofauti kubwa kati ya namna wanaume na wanawake wanavyo weza kujielezea matatizo yao na kuyatatua.
''wanawake huwa wanatumia njia za kujieleza ambazo ni rahisi watu kumuokoa tofauti na wanaume''
Jack anasema ”Natamani kujua nini kilimpata baba yangu kwani fumbo hili linaweza jibu maswali ya familia nyingi wenye matatizo kama yangu”.